We capture your memories forever.

Thursday, June 22

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA RASMI MRADI WA MAJI WA RUVU JUU MLANDIZI MKOANI PWANI PIA AZINDUA VIWANDA VINGINE MKOANI HUMO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Balozi wa India hapa Nchini Sandeep Arya, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa wa Pwani na Serikali akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mradi Mkubwa wa Maji wa Ruvu Juu Mlandizi Mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge mara baada ya kuzindua rasmi Mradi wa huo wa Upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji Ruvu juu Mlandizi Mkaoni Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Archard Mutalemwa mara baada ya kuzindua mradi huo Mkubwa wa maji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia hatua za usafishaji wa maji katika kituo cha kusafisha maji ya Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani, kushoto ni Mtendaji mkuu wa DAWASCO Eng. Cyprian Luhemeja akitoa maelezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma pamoja na Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya mara baada uzinduzi wa mradi huo mkubwa wa kusafisha na kuzalisha Maji kwa miji ya Pwani na Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ujumbe aliotumiwa na Waziri mkuu wa India Narendra Modi kupitia Luninga kabla ya kudua Mradi huo wa maji.

Sehemu ya Mradi huo wa maji wa Ruvu juu Mlandizi Mkoani Pwani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Mfuko wa sandarusi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo kabla ya kuzindua kiwanda cha Global Packing kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilijaribu Trekta mojawapo katika kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage kabla ya kufungua kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeperusha bendera kuashiria kuiruhusu treni ta TRL kusafirisha nondo kutoka kwenye kiwanda cha Nondo cha Kilua Steel Group kilichopo Mlandizi mkoani Pwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine akifungua kiwanda hicho cha nondo.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi kwenye sehemu ya kiwanda cha kutengeneza matrekta URSUS kilichopo Kibaha mkoani Pwani.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuzindua Mradi wa maji wa Ruvu juu Mlandizi mkoani Pwani.
PICHA NA IKULU

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA NGAZI ZA JUU WA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA










Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa zamani wa nchi ya Georgia Mhe. Mikheil Saakshvili akihutubia na kutoa uzoefu wa nchi yake dhidi ya mapambano dhidi ya rushwa wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakiangalia kitabu kinachoelezea mapambano dhidi ya rushwa na Rais wa zamani wa nchi ya Georgia Mhe. Mikheil Saakshvili (kushoto) wakati Ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.
Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.




BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali haitarudi nyuma kamwe katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini mpaka hapo vitendo hivyo vitakapokoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa Kimataifa wa ngazi ya Juu wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Rushwa katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa vita ya kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi ni kipaumbele cha kwanza katika Serikali ya awamu ya Tano na wale wote wanaowezesha, kunufaika na kuhusika na vitendo hivyo wataendelea kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo nchini.

“Kupambana na rushwa ni jambo la msingi na muhimu kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu katika nchi yeyote Duniani,” Amesisitiza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu Tano chini ya Uongozi Shupavu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inaendelea kukaza kamba katika mapambano dhidi ya rushwa ambayo kwa muda mrefu sasa yamechangia kurudisha nyuma juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Amesema Serikali ya Tanzania inalenga kufikia kipato cha kati na kuimarisha uchumi wa viwanda hadi ifikapo mwaka 2015 hivyo malengo hayo yatafanikiwa haraka iwapo tu vitendo vya rushwa vitakomeshwa katika ngazi zote nchini.

Rushwa ni baya na imeharibu sana maisha ya watu na maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hivyo ni lazima ikomeshwe ili jamii iishi maisha mazuri“Ameeleza Makamu wa Rais.

Amesema kuwa hakuna nchi yeyote ambayo haijagushwa na misukosuko ya vitendo vya rushwa Duniani lakini Bara la Afrika limeendelea kuteseka sana na vitendo hivyo kwa miongo kadhaa sasa hivyo jitihada za pamoja zinatakiwa katika kutokomesha vitendo hivyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa wizara yake itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali kwa watumishi wa umma watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa kwenye maeneo yao ya kazi.

Naye, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia bi Bella Bird amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano za kupambana na vitendo vya rushwa na kusisitiza kuwa Benki hiyo ataendelea kutoa mchango wake wa hali na mali katika kuisaidia Tanzania katika uimarishaji wa mapambano hayo.

Mkutano huo wa Kimataifa wa ngazi ya Juu wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Rushwa unaofanyika nchini unahudhuriwa na viongozi mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi wenye uelewa na uzoefu katika mapambano dhidi ya rushwa.

Prof. Maghembe Amuaga Egon Konchane



Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Waziri Maghembe alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano na misaada mbalimbali aliyoitoa, yeye binafsi na nchi yake katika kusaidia kuendeleza sekta ya uhifadhi nchini.

Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (katikati) akifurahia zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori alivyopewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi. Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki.

Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous mkoani Morogoro.
Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kulia) akimkabidhi Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe zawadi ya picha ya kumbukumbu ambayo ilipigwa wakati wawili hao wakitua kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Matambwe, Selous, Kwa mujibu wa balozi huyo siku hiyo haikuwa rahisi kwa ndege hiyo kutua kwa kuwa mvua zilikuwa zinanyesha. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

Sunday, June 18

Highlands255 Teacher's Camp & Conference June 2017 in Morogoro


Picha Zote na Gadiola Emanuel, PICHA ZINGINE ZITAWAJIA HIVI PUNDE...STAY TUNED, STAY WATCHING...




























ANGALIA VIDEO HAPA CHINI