We capture your memories forever.

Thursday, September 28

WATANZANIA WAMETAKIWA KUENZI UTAMADUNI WETU KUKUZA FURSA ZA UTALII WA KIUTAMADUNI


Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbulu


Watanzania wametakiwa kuenzi mila na desturi ambazo ni chanya wazitunze na kuzitumia ili kujenga jamii yenye maadili mema nchini kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipotembelea Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom wilaya Mbulu mkoani Manyara ambapo amejionea utajiri wa kiutamaduni wenye fursa za utalii wa kiutamaduni.


“Nimetembelea nyumba za asili zilizopo hapa katika kituo hiki nimefurahishwa sana na utajiri wa kiutamaduni uliopo hapa, wazee walizingatia maadili katika kuwalea watoto wao kulingana na mila na desturi zao, ni vema tuenzi utamaduni wetu, huo ni msingi wa maadili mema ya jamii” alisema Naibu Waziri Wambura


Akitolea mfano wa maadili mema yanayopaswa kurithishwa aliyojionea katika kituo cha 4CCP na namna ambavyo watoto waliheshimu nyumba za wazazi wao, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa kwa mujibu wa mila na desturi za Kitanzani suala la ulevi na utumiaji wa tumbaku kwa vijana ilikuwa ni mwiko hadi kijana afikie umri wa utu uzima ambapo anaweza kuwa na maamuzi sahihi katika maisha yake yenye kuwa na tija kwa familia.


“Kabla ya kuoa kijana alikuwa haruhusiwi kutumia tumbaku na kunywa pombe, bali kijana akioa na kuwa na watoto wawili kwa mujibu wa mila za makabila ya yaliyopo Mbulu aliruhusiwa kuingia katika kundi la watu wazima na kuruhusiwa kutumia vitu mbalimbali ikiwemo tumbaku na kinywaji cha pombe. Hapa kuna jambo la Watanzania kujifunza na kutunza ili kuondokana na mmomonyoko wa maadili” alisema Naibu Waziri Wambura.


Mila za jamii zilizo njema zinapaswa kutunzwa na kuendelezwa ili ziweze kusaidia vijana na jamii kwa ujumla kuweka mawazo yao katika shughuli za maendeleo pamoja na kupatia familia zao mahitaji ya kila siku.


Naibu Waziri Wambura alisisitiza kuwa mila hizo hazitakiwi kuachwa bali zainatakiwa kuenziwa, kutunzwa, kuendelezwa na kuhifadhiwa kwa manufaa ya sasa ziweze kuchangia katika kukuza utalii wa kiutamaduni ambao ni moja ya vyanzo vya mapato kwa wanajamii na taifa kwa ujumla.


Aidha, Naibu Waziri Wambura alisema kuwa wilaya ya Mbulu ni tajiri katika masuala ya utamaduni na kuongeza kuwa wilaya hiyo ni mdau muhimu katika sekta ya michezo na utamaduni ambazo zinapaswa kuendelezwa kwa manufaa ya taifa.


Kwa upande wake Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay amesema kuwa wilaya hiyo imekuwa na utamaduni wa kufanya tamasha la utamaduni kila mwaka ambapo mwaka huu lilifanyika tarehe 21 hadi 23 mwezi Septemba na inaedelea kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo hatua inayopelekea makabila yote kuwa mstari wa mbele katika kudumisha amani ya nchi.


Mbunge huyo aliyataja makabila yanayotokana na makundi makuu manne yanayopatikana wilaya ya Mbulu kuwa ni pamoja na Wairaqw ambao ni jamii ya Wakushi, Wahadzabe jamii ya Khoisan, Wanyiramba na Wanyisanzu jamii ya wabantu na Wadatooga jamii ya Kiniloti.


Naye Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga amemhakikishia Naibu Waziri Wambura kuwa wilaya hiyo itaendelea kuenzi sekta ya utamaduni kwa kuwa na tamasha la utamaduni linalokutanisha makabila yote wilyani humo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uanuwai wa Utamaduni duniani ambayo hufanyika mwezi Mei tarehe 21 kila mwaka.


Hatua hiyo inatokana na Tanzania kusaini mkataba wa azimio la Umoja wa Mataifa (UN) kuenzi utamaduni na kuheshimu tamaduni za watu wengine chini unaosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).


Mwaka 2002 Umoja wa Mataifa uliamua kuanzisha maadhimisho ya siku ya Utamaduni Duniani kutokana na kuongezeka kwa migogoro, mapigano na kupotea kwa maisha ya watu na mali zao iliyokuwa inatokea sehemu mbalimbali duniani mwishoni mwa miaka ya 1990.



Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa pili kushoto) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi na Usalama mara baada ya kuwasili Wilayani Mbulu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani humo.

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura kuongea na wananchi waliokuwa katika tamasha la utamaduni katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom mara baada ya kuwasili Wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani humo.

Baadhi ya Washiriki wa tamasha la utamaduni katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom, wilaya ya Mbullu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (hayupo pichani) alipotembelea kituo hicho.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akitoka ndani kujionea moja ya nyumba za asili ya Wabantu Wanyiramba na Wanyisanzu iliyopo Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.


Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akicheza ngoma na washiriki wa tamasha la utamaduni alipotembelea Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa pili kulia) akipata maelezo ya utamaduni wa kabila la Wadatoga katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wasichana wa kabila la Datoga na kusisitiza Watanzania kuenzi utamaduni wetu kwa kuurithisha kwa vijana wetu. Wa nne kushoto ni Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay.(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbulu)

MAKAMISHNA WA UPELELEZI WA KODI AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA DAR



Kaimu Naibu Kamishna Upelelezi wa Kodi, Eustacio Makala akisalimiana na Meneja Elimu kwa mlipa kodi, Diana Masala kabla ya kuanza kwa mkutano wa watendaji waandamizi wa Mamlaka za mapato za jumuiya ya Afrika Mashariki kwa makamishna wapelelezi kwa maswala ya kodi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs)

Washiriki wa mkutano huo wakianza kwa kumtanguliza Mungu kwanza.

KAIMU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gerald Mwanilwa akisoma hotuba ya Kamishna Mkuu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa makamshina na watendaji waandamizi wa Mamlaka za mapato za jumuiya ya Afrika Mashariki kwa makamishna wapelelezi kwa maswala ya kodi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
KAIMU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gerald Mwanilwa (kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya watendaji waandamizi wa mamlaka hiyo wakati wa mapumziko ya Mkutano wa Mamlaka za mapato za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa makamishna wapelelezi kwa maswala ya kodi uliofunguliwa jijini Dar es Salaam Septemba 27 2017. Kutokea (kushoto) ni Kaimu Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Kodi, Salim Kessi, Kaimu Naibu Kamishna Upelelezi wa Kodi, Eustacio Makala na Meneja Elimu kwa mlipa kodi, Diana Masala.

KAIMU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Gerald Mwanilwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.

Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano huo.

Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano huo.

SERIKALI YAIPONGEZA COSTECH-OFAB KWA KUANDAA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZA SAYANSI 2017



Mwandishi wa Habari wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu akipeana mkono na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako baada ya kukabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza kwenye kuandika na kuelimisha umma kuhusu matumizi ya sayansi, Teknolojia na ubunifu hususani Bioteknolojia katika kuendeleza kilimo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda

Washindi wa tuzo hizi wakisubiri kutangazwa.

Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz akitoa hutuba katika hafla hiyo.

Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyindondi akielezea tuzo hizo

Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda akizungumzia tuzo hizo

Waziri Ndalichako akihutubia katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk.Ayoub Rioba akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mshindi wa tuzo hizo kutoka mkoani Kagera, Benson Eustace wa Clouds Media kikabidhiwa cheti chake.

Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz akikabidhiwa cheti kutokana na mchango mkubwa wa vyombo hivyo katika kuandika habari za sayansi.

Mwakilishi wa TBC, akikabidhiwa cheti kutokana na mchango wa kuandika habari za sayansi.

Ofisa Mawasiliano wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha SUA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Kujiendeleza (ICE), Bujaga Inzengo Kadago akipokea cheti kutokana na mchango wa vyombo vya habari vya chuo hicho wa kuandika habari hizo.

Mwanahabari wa gazeti la Habari Leo, Lucy Ngowi akikabidhiwa cheti.

Mwanahabari Hellen Kwavava akikabidhiwa cheti.

Mwanahabari wa Gazeti la Nipashe mkoani Kagera, Restuta Damian akipokea cheti.

Mwanahabari wa gazeti la Guardian, Daniel Simbei akipokea cheti.

Mwanahabari Calvin Gwabara kutoka SUA akipokea cheti.

Mwanahabari wa gazeti la Daily News, Fatma Abdul akipokea cheti.

Mwanahabari Elias Msuya wa Gazeti la Mwananchi akikabidhiwa cheti.

Mwanahabari wa RFA kutoka Mwanza, Coleta Makulwa akipokea cheti

Mwanahabari wa gazeti la Habari Leo, Shadrack Sagati akikabidhiwa cheti.
Mwanahabri Dino Mugunde wa Star TV Mwanza akipokea cheti.

Waziri Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na washindi.
Mshindi wa kwanza wa tuzo hizo, Gerald Kitabu akitoa shukurani zake.

Mwanahabari Calvin Gwabara kutoka SUA, akipongezwa na dada yake huku akionesha vyeti vyake.






Na Dotto Mwaibale


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka waandishi wa habari nchini kutumia taaluma zao kuelimisha jamii kuhusu habari za sayansi na teknolojia ili kuleta maendeleo nchini.


Akizungumza wakati wa utoaji tuzo za umahiri katika uandishi wa habari za Sayansi zilizoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknlojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknojia (OFAB), Waziri Ndalichako alisema tuzo hizo iwe ni chachu za kuandika habari za sayansi kwa undani ili kuwajengea uelewa wananchi wa.kawaida.


Alisema ufundi wa waandishi katika.kuandika habari za sayansi utasaidia kutangaza ubunifu na kuongeza tija thamani katika teknolojia mbalimbali."Wananchi wanahitaji teknolojia za kisasa katika kurahisisha utendaji kazi hivyo uandishi wenu utasaidia kuinua sekta ya kilimo na mifugo ambayo ndio kundi.muhimu katika jamii hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda,"alisema Ndalichako.


Aliwataka Costech na taasisi nyingine kuendelea kushirikiana na wanahabari kuelimisha jamii katika masuala ya sayansi.Ndalichako alipongeza COSTECH na OFAB kwa kuandaa tuzo hizo kwani zitaongeza mori kwa wanahabari wa kuandika habari za sayansi.


Akielezea ushiriki wa.waandishi katika shindano hilo lililoanza Januari hadi Agosti mwaka hii, Mkurugenzi Mkuu wa COTECH, Dk.Hassan Mshinda alisema, shindano hilo hapa nchini sasa ni mara ya tisa kufanyika na kwa upande wa Afrika ni la kumi.


Alisema katika shindano hilo jumla ya makala 200,vipindi vya radio 20 na televisheni 15 vilishindaniwa.Mshindi alisema watalaam waliobobea ambao walifanyakazi ya.kutafuta washindi ambao walipata dola 250, 750, 1,000 na 1,500.Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Jim Yonaz aliwataka waandishi kuwa daraja kati ya wana sayansi na jamii.


Alisema wana sayansi wana lugha ngumu hivyo kupitia waandishi na aina ya uandishi wao wamesaidia jamii kuelewa habari mbalimbali za sayansi."Katika kuchangia uchumi wa viwanda waandishi wanakazi kubwa kuhakikisha wanatoa elimu ya sayansi na kilimo ili kuelimisha jamii,"alisema Yonaz.


Yonaz pia aliiomba Serikali kuhakikisha inawawezesha waandishi kwa kuwajengea uwezo wa ufahamu ili waweze kuelewa zaidi sababu zinazowafanya kuandika habari mbalimbali.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk.Ayoub Rioba alisema, wana sayansi wana jukumu la kuboresha maisha ya jamii kwa kuhakikisha wanatumia zana zilizoboreshwa kiteknolojia.Alisema kwa sababu ya lugha itumikayo na wana sayansi upo umuhimu wa wanahabari kuandika.habari nyingi za sayansi.


Rioba pia aliitaka taasisi ya Costech pamoja na taasisi nyingine kuendelea kufanya kazi za kuelimisha jamii kwa kushirikiana na wana habari ili kujenga jamii yenye uelewa wa masuala ya sayansi.Miongoni mwa waliopata tuzo za umahiri wa habari za Sayansi ni pamoja na mshindi wa jumla Gerald Kitabu (Guardian), Shedrack Sagati(Habari Leo), Elias Msuya (Mwananchi), Calvin Gwabara, Fatma Abdul (Daily News) na Dino Mugunde.


Wengine ni Lucy Ngowi, Hellen Kwavava, Coleta Makulwa, Daniel Simbei, Benson Eustace na Restuta Damian.

GLOBAL PUBLISHERS WATOA ZAWADI KWA MSHINDI


Diwani ya Kata ya Mabibo (aliyefungwa kitambaa machoni), akipelekwa na MC wa shughuli hiyo, Chaku kwenda kuchagua kuponi ya ushindi. Mheshimiwa diwani akiwa kwenye rundo la kuponi Mheshimiwa diwani akichanganya kuponi. Kazi ya kuchanganya kuponi ikiendelea. Mheshimiwa diwani akiwa ameshika kuponi ya ushindi, iliyotoka Gazeti la Championi. Mheshimiwa diwani akiwa ameiinua kuponi juu. Diwani Lema akisoma jina la mshindi wa nyumba, aliyemshikia kipaza sauti ni MC Chaku. Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akizungumza kwenye droo hiyo kubwa ya Shinda Nyumba. Meneja Mrisho akipeana mikono na Diwani Lema Diwani Lema akizungumza na watu waliofika kushuhudia droo hiyo. Msomaji akichagua kuponi ya mshindi wa zawadi ya dinner set. Msomaji akichagua kuponi ya mshindi wa zawadi ya dinner set. Mhariri wa Uwazi, Elvan Stambuli (kulia) akiwa na mhariri mwenzake, Sifael Paul anayesimamia Gazeti la Ijumaa Wikienda. Abdallah Hemed (kushoto), afisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, akiandika jambo huku akifuatilia droo hiyo, pembeni yake ni Meneja Mrisho.