Northern Shots Media

We capture your memories forever.

Sunday, June 10

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AWAVISHWA VYEO MAOFISA WAANDAMIZI TISAWA JESHI LA MAGEREZA JIJINI DAR






Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akimvalisha cheo akimvalisha cheo Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila kuwa Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 8, 2018.

Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kulia) akimvalisha cheo Mkuu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga kuwa Naibu wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 8, 2018.

Makamishina na Manaibu Kamishna wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam leo Juni 2, 2018.



Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt Juma Malewa akikagua gwaride maalum katika hafla ya uvishaji vyeo kwa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.

Baadhi ya Maafisa Wastaafu na waliopo sasa wa Jeshi la Magereza wakifuatilia hafla fupi ya uvishaji vyeo kama inavyoonekana katika picha.

amishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza waliowavalisha vyeo hivyo kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli ambapo hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni, 8, 2018.Picha zote na Jeshi la Magereza






KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa, kwa niaba ya Amiri jeshi mkuu Rais John Magufuli amewavisha vyeo maafisa wa ngazi ya juu 9 wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Miongoni mwa maafisa 9 waliovishwa vyeo ni manaibu kamishna wa magereza – DCP wanne wa Jeshi hilo ambao wamepandishwa vyeo na kuwa Makamishna wa magereza, huku makamishna wasaidizi waandamizi wa Magereza -SACP watano wakipandishwa vyeo kuwa Manaibu Kamishna – DCP wa Jeshi hilo.


Waliovishwa vyeo kuwa Makamishna wa Magereza ni Naibu Kamishna wa Magereza Uwesu Ngarama, Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza Tusekile Mwaisabila, Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Urekebishaji, Naibu Kamishna wa Magereza Augustine Mboje, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Naibu Kamishna wa Magereza Gideon Nkana ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam.


Wengine waliovishwa vyeo kuwa Manaibu Kamishna wa Magereza ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Julius Sang’udi, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Afwilile Mwakijungu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, John Masunga, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Phaustine Kasike, Mkuu wa Kitengo cha Parole pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Jeremiah Katungu ambaye ni Katibu Ofisi ya Kamishna Jenerali wa Magereza.


Akizungumza mara baada ya kuwavisha vyeo Maafisa hao wa magereza(Ijumaa, Juni 8, 2018) katika hafla ya kuwavisha vyeo hivyo iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa amewataka makamishna hao wa Jeshi la magereza wa ngazi zote kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uadilifu sambamba na kusimamia haki na usawa katika utekelezaji wa majukumu yao kila siku.


Aidha, Jenerali Malewa amemshukru Amiri jeshi mkuu Rais John Magufuli kwa kuwapandishwa vyeo maafisa hao ambao watajaza nafasi mbalimbali za juu za uongozi ndani ya Jeshi la Magereza kwani kwa muda mrefu safu ya juu ya uongozi ilikuwa na upungufu mkubwa wa kada ya maafisa wa vyeo hivyo hali iliyopelekea kuathiri utendaji kazi wa Jeshi hilo.


Maafisa hao kabla ya kuvishwa vyeo hivyo walivyotunukiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuanzia Juni 02, 2018, walipata fursa ya kula kiapo cha Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma mbele ya katibu wa sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma.

Sunday, May 13

JUMIA YATOA SAMSUNG S9 NA S9+ KWA WATEJA WAKE



Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott , akimkabidhi simu ya Samsung Galaxy S9, mteja Happiness Keto aliyoinunua simu hiyo kwa shilingi 59,000 tu katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Mteja Happiness Keto akionesha simu hiyo kwa waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott , akimkabidhi simu ya mwakilishi wa mteja wa Lumby Elia aliyoinunua simu hiyo aina ya Samsung Galaxy S9+ kwa shilingi 81,000 pekee!
Mwakilishi wa mteja wa Lumby Elia akionesha simu hiyo kwa wanahabari.


Meneja Uhusiano wa Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mteja Happiness Keto akizungumza kwenye mkutano huo.






JUMIA imekabidhi simu mbili za Samsung Galaxy S9 na S9+ kwa wateja wake wawili ambao waliibuka washindi kupitia zoezi la kusaka simu kwenye mtandao wao (Treasure Hunt) kupitia kampeni ya ‘Mobile Week.’

Katika zoezi hilo wateja waliofanikiwa kuzipata simu hizo zilizofichwa, walipewa ofa ya kuzinunua kwa bei ya chini kupindukia tofauti na gharama yake halisi. Baada ya kufanikiwa kufanikiwa kuipata simu ya Samsung Galaxy S9, mteja Happiness Keto aliinunua simu hiyo kwa shilingi 59,000 tu, wakati mwenzake Lumby Elia yeye aliinunua Samsung Galaxy S9+ kwa shilingi 81,000 pekee!

Bei halisi ya simu ya Samsung Galaxy S9 ni shilingi 2,049,000 ikiwa imepunguzwa kutoka shilingi 2,500,000 wakati Samsung Galaxy S9+ ni shilingi 2,315,000 nayo ikiwa imepunguzwa kutoka shilingi 2,800,000! Hivyo unaweza kujionea ni kwa namna gani wateja hawa walivyokuwa na bahati!

Simu hizi zilizinduliwa mapema mwezi Februari mwaka huu na kampuni ya Samsung duniani ambapo kwa hapa nchini Tanzania ilikuwa ikipatikana kwa malipo ya kabla kupitia kwenye mtandao wa Jumia pekee.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa simu yake ya Samsung Galaxy S9+, Lumby Elia amesema kuwa ana furaha sana hatimaye kuishika simu hiyo mkononi kwa mara ya kwanza kwani ni kama ndoto kuinunua kwa bei hiyo kwa sababu ni sawa na bure.

“Ni ndoto ya watu wengi kumiliki bidhaa ambayo ni toleo jipya hususani kama simu ambazo kila mwaka huwa zinakuja na matoleo na maboresho tofauti. Simu hii kwangu mimi ni kama ndoto kutokana na ubora na thamani yake pamoja na uwezo ilionao,” alisema na kumalizia Bi. Elia, “Naishukuru sana Jumia kwa zawadi hii lakini pia kwa fursa iliyoitoa kwa wateja wake kuweza kutumia bidhaa halisi na mpya kabisa iliyoingia kwa mara ya kwanza sokoni. Nawasihi wateja wengine wakiona fursa kama hizi wasizipuuzie, ni kweli kama hivi mnavyoona.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Tanzania, Bw. Zadok Prescott ameongezea kuwa ni madhumuni ya kampuni yake kuona inabadili utamaduni wa Watanzania katika kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao.

“Nafahamu kwamba bado Watanzania wengi wana hofu ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao. Kwa sababu wengi wao wamejaribu kulaghaiwa mara kadhaa walipojaribu kufanya hivyo. Lakini ningependa kuwahakikishia mambo ni tofauti kwa Jumia. Jumia ni sehemu PEKEE inayokuhakikishia bidhaa halisi. Unaweza ukaagiza bidhaa, halafu ukalipia mara baada ya kukufikia, tena ukiwa umeridhika nayo. Hata baada ya kununua bidhaa, halafu ukabadili mawazo yako ndani ya siku 7, ikiwa bado haijafunguliwa wala kutumika, ikakurudishia pesa zako - hata gharama za kusafirisha! Hata namna ya kufikiwa na bidhaa yako ni haraka pia! Inachukua takribani muda wa siku 2 tu kwa bidhaa zinazoagizwa ndani ya jiji la Dar es Salaam,” alifafanua Prescott.

“Kuonesha kwamba tunawajali wateja wetu, Jumia leo inazindua rasmi kampeni nyingine ya ‘Mobile Week.’ Safari hii ikiwa imeboreshwa zaidi kwa ofa, mapunguzo ya bei na zawadi kemkem kwa wateja,” alisema Prescott na kuhitimisha kuwa, “kitu cha kusisimua zaidia, tunafahamu kuwa kwa mashabiki wengi wa mchezo wa mpira wa miguu macho na masikio yote wametega kuelekea kuanza kwa Kombe la Dunia. Jumia hatutowaacha watupu, tuna kampeni kubwa pia itakuja siku si chache pamoja na nyinginezo nyingi zitakazokuwa zikiendeshwa kila wiki.”

Dkt Kalemani azindua Baraza la Kwanza la Wizara ya Nishati





Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amezindua Baraza la Kwanza la Wizara ya Nishati na kutoa maagizo mbalimbali kwa Watendaji wa Wizara na Taasisi ili Sekta ya Nishati iendelee kuwa injini katika ukuaji wa uchumi.

Dkt. Kalemani amezindua Baraza hilo tarehe 11 Mei, 2018 mkoani Dodoma ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria uzinduzi huo akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye alimwakilisha Katibu wa TUGHE Taifa na Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya.

Akizungumza na Wajumbe wa Baraza, Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Wajumbe wa TUGHE, Tawi la Wizara ya Nishati, Dkt. Kalemani alisema kuwa, jukumu kuu la Wizara na Taasisi zake ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata nishati ya umeme ya kutosha hivyo wana jukumu la kutafakari namna ya kutekeleza suala hilo.

Dkt. Kalemani, aliwaagiza watendaji wa Wizara na Taaisi kuhakikisha kuwa kunakuwepo na miundombinu ya kutosha ya kusafirisha umeme ili umeme unaozalishwa uweze kuwafikia wananchi kwani kuna sehemu ambazo umeme umekuwa ni mwingi kuliko matumizi ya nishati hiyo. Aidha, Dkt Kalemani aliwataka watendaji hao kuhakikisha kuwa, wananchi waliolipia huduma ya umeme, wanaunganishwa na huduma hiyo ndani ya wakati ambao ni siku Saba.

Vilevile Dkt. Kalemani, alisema kuwa, kila mtendaji ana jukumu la kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Kuhusu masuala yanayohusu Watumishi, Dkt Kalemani aliagiza kuwa watumishi wanaokaimu nafasi mbalimbali kwa muda mrefu wathibitishwe katika nafasi hizo ili watumishi hao watekeleze majukumu yao kwa kujiamini na kuwa na ari.

Waziri wa Nishati pia aliagiza kuwa, watumishi wapandishwe madaraja kama inavyostahili ili kuwapa morali ya kufanya kazi, pia motisha na mafunzo sehemu ya kazi yaendelee kutolewa ili kuwajengea uelewa watumishi na hivyo kuleta ufanisi katika Sekta wanayoisimamia. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, pamoja na kupongeza ushirikiano anaopata kutoka kwa Watendaji wa Wizara na Taasisi katika majukumu yake ya kila siku, aliwataka watendaji hao kuhakikisha kuwa maagizo yote yaliyotolewa na Waziri wa Nishati yanatekelezwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua alisema kuwa Baraza hilo la Wafanyakazi ni muhimu kwani pamoja na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Watumishi, pia litajadili utekelezaji wa miradi ya Sekta ya Nishati kwa mwaka 2017/2018 na mipango ya maendeleo kwa mwaka 2018/2019. Vilevile alisema kuwa, Baraza hilo litajadili Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2017/18 na litapitia Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2018/19.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa pili kushoto), Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye ni mwakilishi wa Katibu wa TUGHE Taifa (wa kwanza kulia), Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya (wa kwanza kushoto) na Katibu Mpya wa Baraza la Wafanyakazi, Wizara ya Nishati, Pascal Mduma (wa pili kulia) wakiimba wimbo wa Mshikamano wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika mjini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati), Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala, Tabu Mambo, ambaye ni mwakilishi wa Katibu wa TUGHE Taifa (kulia) na Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya (kushoto) wakiimba wimbo wa Mshikamano wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati uliofanyika mjini Dodoma.


Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake wakiimba wimbo wa Mshikamano katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma tarehe 11 Mei, 2018.


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti (waliosimama) iliyoandaa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati kilichofanyika mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua na kushoto kwake ni Katibu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, John Mchenya.


Watendaji kutoka Idara ya Utawala na Rasilimali Watu na Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Nishati wakiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma tarehe 11 Mei, 2018.


Watendaji mbalimbali wa Wizara ya Nishati wakiwa katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika mjini Dodoma tarehe 11 Mei, 2018.

Saturday, January 6

WAZIRI UMMY AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA KLABU YA AFRICAN SPORTS



WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu katikati akimkabidhi vifaa vya michezo ambavyo ni viatu Mwenyekiti wa timu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba ikiwa ni kuipa motisha timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano wanayoshiriki ili waweze kufanya vizuri na hatimaye kuweza kurejea daraja la kwanza na Ligi kuu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports Awadhi Salehe Pamba leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Meja Hamisi Mkoba



Halfa ya makabidhiano ikiendelea

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kushoto akimkabidhi viatu hivyo Nahodha wa timu ya African Sports Mohamed Kidiwa






WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ametoa vifaa vya michezo kwa timu ya African Sports ya Tanga yenye thamani ya zaidi ya milioni 1.5 ikiwa ni mkakati kabambe wa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki na hatimaye kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao.


Makabidhiano hayo yalifanyika leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga wakati wa ufunguzi wa timu ya wanawake ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya wilaya ya Tanga ambapo alisema vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya timu hiyo kuweza kufikia malengo yao.


Aliyasema hayo mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa timu hiyo katika halfa iliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa klabu ya African Sports ambapo alisema dhamira yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inarejea ligi daraja la kwanza na ile ya Coastal Union ihakikisha msimu ujao inarudi Ligi kuu.


“Niseme tu sisi tumejipanga kuhakikisha tunazirejesha timu hizi kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara tukianzia na timu ya Coastal Union lakini ndugu zangu African Sports mhakikishe mnarudi ligi daraja la kqwanza na baadae ligi kuu “Alisema


Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo,Mwenyekiti wa Klabu ya African Sports,Awadhi Salehe Pamba alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwasaidia msaada huo ambao utakuwa ni chachu kwao kuweza kufikia malengo yao kutokana na changamoto hiyo kwisha.


Alisema msaada uliotolewa na Waziri utakuwa chachu kubwa kwao kuweza kufikia malengo yao waliojiwekea ya kuhakikisha wanarudi ligi kuu kwani ndio ndoto yao kubwa ambayo wamekuwa wakiiwaza kila wakati.


“Mh Waziri tukushukuru sana katika hili umetupa nguvu ya kuweza kupambana na tuna kuhaidia kuhakikisha tunairudisha timu Ligi daraja la kwanza na hatimaye ligi kuu.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Zanzibar to Organize a Half Marathon race to Promote Gender Mainstreaming, Attain Sustainable Development Goal



More than 300 Zanzibari women, men, girls and boys are expected to participate in the race ZANZI HALF scheduled to take place on February 4th, 2018 in Stone Town in the Isles.
ZANZI HALF is an international standard sporting and cultural event featuring a half marathon of 10 km and 5 km distances to be staged for the first time in the East African archipelago of Zanzibar with ethe view to highlighting women's empowerment and gender equality.
The race is a response to the 2030 agenda for sustainable development with a call out for action in the world, and is organized by the local interfaith women´s program Upendo Means Love and the Danish NGO and running community Right to Movement in collaboration with ZIFF, Zanzibar International Film Festival (ZIFF) and Zanzibar Amateur Athletic Association (ZAAA).
Women and girls are at the very heart of the agenda in an acknowledgement that their participation is crucial as a pre-condition for the achievement of sustainable development, says one of the organizer,Ms Lotte Bredholt. The race will bring together women and men from the grass root level united in a movement that will translate into further action, transforming gender norms by challenging existing traditional roles, taboo and break down stereotypes showing women and girls as active agents of change and peace. However, sustainability and equality is only achievable if women and men work together.
“Running is empowering” continues Lotte Bredholt, “when women and girls realize their potential and strength on the track and on the streets, there is a spillover effect to other areas of life”. Running is a tool as well for inter-community dialogue continues Lotte Bredholt. Besides the race event, ZANZI HALF encourages local society, rural and urban, to take up running and to be part of a running community. In the meeting between people, sharing experience and passion for a common activity, socio cultural, religious and gender barriers diminish. “It´s a commitment to enhance diversity and inclusion, and is part of the global agenda for sustainable development”.
Fumba Town Development, a project by CPS (FTD),issponsoring the event as part of their support for socio-economic development in Zanzibar. Fumba Town Development combines state-of-the-art residential properties, based on a modern and sustainable infrastructure, with commercial, educational and recreational areas to create a new, modern lifestyle in Zanzibar.
As part of our community development initiatives, we are proud to have teamed up with Zanzihalf for their initial half-marathon on February 4th. We are very excited about the upcoming event and are already training as Fumba Town Team to take part in the race. With regular participants of about 30 runners from our company and the villagers around, we already make an impact towards bringing the communities together.
The Zanzibar Amateur Athletic Association welcomes a race which brings awareness to the role of sport empowering women, however as MlingiBwire points out, a proper half marathon also should have cash prices to attract the elite runners. Though not big, the tree first runners from the two distances 10k and half marathon will be rewarded with a price. All participants will receive a medal.
About the partners
Upendo Women Empowerment is a non-for-profit faith based womens program and social enterprise established in 2005 with the mission of bringing women and girls of different faith together to promote solidarity, trust and peace and to fight poverty by empowering women through vocational training and employment. The vision is a Zanzibar where empowered women and men of different faith contribute to an equal, just and peaceful society, a society where women and men are ready to stand up for human rights, social and economic prosperity and thereby increase equal opportunities in life. In doing so, women and men in Zanzibar become an example of peaceful coexistence and respect between people of different faith.
Right to Movement is a global running community with a growing number of runners, races and communities all over the world running to claim their human right to freedom of movement. RTM is a non-profit, non-religious and non-politic social movement.


Right to Movement came into existence in April 2013, as a conceptual bi-product of the inaugural event Palestine Marathon. Under the slogan “Right to Movement”, RTM held the first ever Palestine Marathon to promote the basic human right to freedom of movement as stipulated under Article 13 in the Human Rights Charter – and to tell a new story about Palestine.


Building on the success of the inaugural Palestine Marathon, Right to Movement establishes running communities and races primarily in countries where the right to free movement is threatened - either for citizens in general or for women in particular. Communities of running activists engaged in the world, with a global and humanitarian outlook who use their love of running to claim their human rights - either for themselves or in solidarity with others. And to inspire others to do the same via their story-sharing on SoMe using the hashtag #righttomovement.In 2016 Right to Movement was awarded as NGO of the year by the organization Sports and Peace in Monaco.


Zanzibar International Film Festival ZIFF also known as Festival of the Dhow Countries is an annual film festival held in Zanzibar. ZIFF is a non-governmental organization established in 1997 and has developed into one of the largest multi-disciplinary art and cultural festival in Africa dedicated to films, music and different form of arts. Over the years, ZIFF has used their platform Women Panorama as a medium of women´s power and visibility to highlight and address pertinent gender and social issues. The Women´s Panorama commonly comprises of a series of workshops, parades, cultural activities, seminars and symposia organized and centered on the visibility of women in and through medium of cinema, the arts and the media.


Registration for the race have started for international and regional participation on the website zanzihalf.com and locally in Stone Town at Upendo Means Love located at Kiponda area, at the heart of the historic stone town. or contact Info@zanzihalf.comt tel +255 (0) 777 120 651. For press contact: Ms. Lotte Bredholt, +255777120561

MKANDARASI WA REA MBEYA NA SONGWE KUCHUKULIWA HATUA






Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini (hawapo pichani) alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza kwenye ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza (kulia aliyesimama) wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini (hawapo pichani) alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Mtinika (aliyesimama) akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kushoto waliokaa) ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiagana na Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza (kulia) mara baada ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Mkoani Mbeya. Kushoto ni Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Benedict Bahati.




Shirika la Umeme Tanzania limeagizwa kumchukulia hatua Mkandarasi ambaye ni kampuni ya wazawa ya JV State Grid Electrical & Technical Works Ltd aliyekuwa akitekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) Mikoa ya Mbeya na Songwe kwa kushindwa kukamilisha katika baadhi ya maeneo kwa mujibu wa makubaliano.


Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa agizo hilo Januari 5, 2018 kwenye mkutano na wananchi wa Kijiji cha Utengule Usongwe, Mbeya Vijijini alipokuwa kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Umeme Vijijini.


Mgalu alitoa agizo hilo kufuatia taarifa ya Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Benedict Bahati ambaye alimueleza kuhusu kampuni hiyo iliyokuwa ikitekeleza Miradi katika Wilaya za Mbarali, Rungwe, Kyela na Ileje kushindwa kukamilisha miradi yake kama ilivyopaswa kulingana na mkataba.


Alisema Serikali haitowafumbia macho Wakandarasi walioshindwa kukamilisha utekelezaji wa Miradi waliyokabidhiwa kwa mujibu wa makubaliano na aliliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha Mkandarasi huyo anapatikana na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa makubaliano ya awali.


“Serikali haijaribiwi, tutachukua hatua kwa Wakandarasi wote walioshindwa kutekeleza Miradi waliyokabidhiwa kwa mujibu wa Sheria; TANESCO na REA, hakikisheni Mkandarasi huyu anapatikana na hatua stahiki za kisheria zinachukuliwa dhidi yake,” alisema Mgalu.


Mgalu aliagiza Mkandarasi huyo apatikane ndani ya Siku Saba ili aeleze sababu za kushindwa kutekeleza mradi huo kwa kiwango kilichokubaliwa na kwa muda wa makubaliano. “Nataka ndani ya Siku Saba tukutane nae aeleze kwanini hajakamilisha mradi kwa mujibu wa mkataba wake,” alisema.


Aliongeza kuwa Serikali imedhamiria kuwainua Wakandarasi wazawa hata hivyo katika utekelezaji wa miradi hiyo ya REA, imedhihirika kwamba walio wengi wameshindwa kutekeleza miradi waliyokabidhiwa kwa mujibu wa makubaliano.Aidha, Naibu Waziri Mgalu alionya Wakandarasi waliopewa jukumu la kutekeleza Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kuhakikisha wanatekeleza kwa mujibu wa mkataba na kwamba Serikali haitomvumilia Mkandarasi atakayekwenda kinyume.


“Wakandarasi mnaotekeleza mradi wa REA III; anayeona hawezi kazi atupishe; hatutomvumilia Mkandarasi anayeharibu kazi,” alionya Naibu Waziri Mgalu.Alisema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Miradi ya Umeme Vijijini inakamilika kwa kiwango kinachokubalika na kwa wakati kama inavyoelekezwa kwenye mikataba waliyoingia na Serikali.


Naibu Waziri Mgalu yupo Mkoani Mbeya kwa ziara ya kukagua na kujiridhisha utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini hususan ya REA pamoja na kuzungumza na Wananchi na Wakandarasi kuhusiana na utekelezaji wake.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA SOKO LA KONDE-PEMBA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipongezana na viongozi wengine mara baada ya ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Sehemu ya wananchi waliohudhuria hafla fupi ya ufunguzi wa soko jipya la Konde lililopo Konde, Micheweni,Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Karume Pemba tayari kwa ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed wakati alipowasili Konde tayari kwa ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud Mohamedmara baada ya kuwasili Konde tayari kwa ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na na Viongozi mbali mbali waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na na Viongozi mbali mbali waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa soko la Konde lililopo Wilaya ya Micheweni, Pemba.


Monday, November 6

DC SHINYANGA ASHIRIKI CHAKULA CHA PAMOJA NA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA






Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishindana kucheza muziki na watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija wakati wa hafla ya kula chakula cha pamoja kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania Limited-Picha na Marco Maduhu - Malunde1 blog




Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameshiriki katika hafla fupi kula chakula cha pamoja na watoto wenye ualbino wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija mjini Shinyanga kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania Limited inayomilikiwa na Crissant Mssipi.


Kabla ya kula cha pamoja na watoto hao,mkuu huyo wa wilaya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo ya ulinzi walifanya usafi wa mazingira ikiwemo kupulizia dawa ya kuua wadudu kama vile kunguni katika mabweni yanayotumiwa na watoto hao.


Hafla fupi ya chakula cha pamoja iliyohudhuriwa pia na Afisa Mthibiti ubora wa Shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga,imenogeshwa kwa burudani ya muziki ambapo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro aliamua kucheza muziki na watoto hao hali iliyoongeza furaha zaidi kwa watoto hao.Akizungumza katika kituo hicho,Matiro ameitaka jamii kuondokana na dhana ya kuwabagua na kuwafanyia vitendo vya kikatili ikiwemo kukata viungo na kuwaua akibainisha kuwa watoto wenye ualbino binadamu kama wengine na kinacho watofautisha ni rangi tu ya ngozi yao.


Amesema jamii ikibadilika watoto hao wataishi kwa amani na furaha kwa kujiona hawana tofauti na binadamu wengine ."Naomba jamii iondokane na matukio ya kuwanyanyasa watoto hawa ili nao waishi kwa amani na upendo ," amesema Matiro.Aidha alisema hivi karibuni serikali iliamua kuwarudisha majumbani baadhi ya watoto waliokuwa wanaishi katika kituo hicho wakiwemo waliohitimu elimu yao ya msingi katika Shule ya Buhaghija hivyo akaitaka jamii kuhakikisha inawalinda na wanaishi kwa amani bila ya kubughudhiwa.


Naye msemaji wa Kampuni hiyo ya Ulinzi Twaha Makani, amesema mara baada ya siku chache kukitembelea kituo hicho waliguswa na vitu vingi vinavyohusu maisha ya watoto hao na hivyo kuamua kufanya shughuli za usafi wa mazingira, kupulizia dawa ya kuua kunguni pamoja na kula nao chakula cha pamoja.


Kwa upande wake mmoja wa walezi wa kituo hicho Bright Mduma mbali na kuishukuru kampuni hiyo ya ulinzi kwa kufanya usafi,kuua wadudu na kuandaa chakula,amesema kituo hicho kina jumla ya watoto 228, watoto wenye ualbino 144, wasiosikia 60 na wasioona 24.Mwandishi wa Malunde1 blog,Marco Maduhu alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha za matukio yaliyojiri.

Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akizungumza katika hafla fupi ya kula chakula cha pamoja na watoto wanaolelewa kituo cha Buhangija Mjini Shinyanga ambapo aliwahakikishia ulinzi pamoja na kuboreshewa makazi yao.-Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

Msemaji wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD inayomilikiwa na Crissant Mssipi, bwana Twaha Makani akizungumza na watoto hao ambapo alisema kampuni hiyo itaendelea kushirikiana nao kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinaendelea kuwakabili.

Msemaji wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD inayomilikiwa na Crissant Mssipi, bwana Twaha Makani akizungumza katika kituo cha Buhangija

Afisa Mthibiti ubora wa shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga, akizungumza na watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija ambapo aliwataka wadau wajitokeze kuwasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili pamoja na kushiriki kula nao chakula cha pamoja na siyo kusubiri hadi siku za sikukuu.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD wakipulizia dawa ya kuua kunguni katika mabweni ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija

Zoezi la kupulizia dawa ya kuua wadudu likiendelea

Sehemu ya Mashuka yakiwa yameanikwa baada ya kufuliwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo

Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akipika chakula kwa ajili ya watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.

Watoto wenye ualbino wakila chakula cha pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ,kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD

Watoto wanaolelewa katika kituo cha Buhangija wakila chakula cha pamoja na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ,kilichoandaliwa na Kampuni ya Ulinzi Cyvalo Tanzania LTD

Watoto wakiendelea kula chakula

Baadhi ya walinzi wa kampuni hiyo nao wakishiriki kula chakula cha pamoja na watoto hao

Zoezi la kula chakula likiendelea

Watoto wakila chakula

Mtoto akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (aliyevaa nguo nyekundu) uwezo wake wa kucheza muziki





Mkuu wa wilaya Josephine Matiro (aliyevaa nguo nyekundu) akicheza muziki wimbo wa Diamond Platnumz zilipendwa na watoto wenye ualbino katika kituo cha Buhangija





Mimi ni nomaaaa!! subiri nikuoneshe kazi mkuu.......





Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akifurahia show ya mtoto.....

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akicheza na watoto hao

Kushoto ni Afisa Mthibiti ubora wa shule halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Aziza Yanga akicheza muziki

Watoto wakicheza mziki wa Kamatia chini

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akicheza Kwaito na watoto hao

Watoto wakicheza muziki na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro

Watoto wakisakata rhumba

Watoto wakiendelea kucheza


Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog