We capture your memories forever.

Showing posts with label Health. Show all posts
Showing posts with label Health. Show all posts

Wednesday, October 11

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MTOTO WA KIKE MKOA WA SHINYANGA OKTOBA 11,2017






Mkoa wa Shinyanga leo umeungana na mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 11 mwezi Oktoba.





Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike katika mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.



Sherehe za maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike yamehudhuriwa na watoto kutoka maeneo na shule mbalimbali mkoani Shinyanga,viongozi wa serikali na vyama vya siasa,wananchi na mashirika na taasisi zisizokuwa za kiserikali likiwemo shirika la kimataifa la Save the Children.



Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu ya “Tokomeza Mimba za utotoni,Tufikie uchumi wa viwanda”.

Akitoa hotuba kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa mitano inayoongoza kwa mimba za utotoni nchini hivyo jitihada mbalimbali zinahitajika kuhakikisha mimba za utotoni zinatokomezwa mkoani humo.



“Ili tufikie uchumi wa viwanda tunahitaji kutokomeza mimba za utotoni ambazo zinachangiwa pia na ndoa za utotoni,ni wajibu wetu serikali,wazazi na wadau wote yakiwemo mashirika na taasisi zinazohusika na masuala ya haki za watoto kuweka nguvu pamoja ili kukomesha vitendo hivi”,alieleza Matiro.



Aidha aliwanyoshea vidole baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakishirikiana na wanaume wanaowapa mimba watoto kwa kumaliza kesi kimya kimya huku wengine wakidiriki kuozesha watoto.

Matiro alitumia fursa hiyo kuliagiza jeshi la jadi sungusungu kuwashughulikia watu wanaowapa mimba watoto huku akitaka elimu zaidi kuendelea kutolewa katika jamii kuhusu haki za watoto.



Matiro pia aliwasisitiza wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao kike na kuwaeleza madhara ya kujiingiza katika mambo ya mapenzi wangali wadogo badala ya kuwaonea aibu huku akiwataka watoto kutokubali kudanganywa na waume ili kuepuka mimba za utotoni.



Naye Meneja wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima alisema vitendo vya mimba na ndoa za utotoni litapungua endapo kesi zinazohusu masuala ya watoto zitachukua muda mfupi kumalizika.



“Bado tuna tatizo la mifumo ya utoaji haki,matukio ya ukiukaji wa haki za watoto yanapotokea,mara nyingi vyombo vya dola ikiwemo polisi wamekuwa wakitumia muda mrefu kufanya uchunguzi,hali hii inatoa mwanya kwa wahalifu kuwapa hongo wazazi watoto kisha kumaliza kesi kienyeji na haki ya mtoto kupotea”,alieleza Malima.



Hata hivyo Malima alishauri kuanzishwa mfumo maalumu kutoa elimu kwa jamii kuhusu haki za watoto utakaosimamiwa na serikali kwa kuyahusisha mashirika na taasisi zinazohusika na masuala ya watoto ili jamii iweze kuondokana na mila potofu zinazogandamiza haki za watoto.



Kwa upande wake,Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal aliwataka akina mama kuwa mstari katika kuhakikisha watoto wanaenda shule na kukataa watoto wao kuozeshwa kwa tamaa ya mali huku akiwasisitiza watoto kusoma kwa bidii na kutokubali kurubuniwa kuacha masomo ama kuambiwa wafanye vibaya katika mitihani yao ili wakifeli waolewe.



Akisoma risala kwa niaba ya watoto wa kike mkoa wa Shinyanga,Rosemary Richard kutoka shule ya msingi Iselamagazi alisema miongoni mwa changamoto zinazowakabili watoto ni jamii kuwa na uelewa mdogo kuhusu haki za watoto.



Alizitaja changamoto zingine kuwa ni mila potofu,watoto kutoshirikishwa katika maamuzi na kutoa mawazo katika familia,kubakwa,kupewa mimbana kukatishwa masomo ili wawe chanzo cha mapato wanapoolewa.



Aliiomba serikali na wadau kutoa elimu kuhusu haki na sera za mtoto huku akiitaka serikali kuwachukulia hatua kali watu wanaowafanyia ukatili watoto lakini pia akaomba katika kila shule kutenga vyumba maalum kwa ajili ya watoto wa kike kujisitiri wanapokuwa katika hedhi.

Mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akitoa hotuba katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini leo Oktoba 11,2017.Picha zote Kadama Malunde- Malunde1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kukataa kurubuniwa ili kuepuka mimba za utotoni.

Watoto wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro huku wakisoma vipeperushi vinavyohusu masuala ya watoto.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa.

Mgeni rasmi Josephine Matiro (katikati ya watoto) akicheza muziki na wanafunzi,aliyevaa nguo nyekundu ni Afisa Utamaduni wa wilaya ya Shinyanga,Janeth Elias,aliyekuwa MC katika maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike.

Meneja wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike kwa mkoa wa Shinyanga ambapo alisema mapambano dhidi ya mimba na ndoa za utotoni yanahitaji ushirikiano baina ya serikali,wazazi na mashirika na taasisi zinazohusika na masuala ya watoto.

Wanafunzi wakifurahia jambo wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike kimataifa.

Meneja wa Shirika la Kimataifa la Save the Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima aliwataka wananchi kuachana na mila na desturi zilizopitwa na wakati ikiwemo ya Chagulaga ambayo wanaume hutumia fursa kuchagua mchumba na kusababisha watoto wa kike waolewa bila ridhaa yao.

Meneja Mradi wa ulinzi wa mtoto, haki za watoto na utawala kutoka shirika la Rafiki SDO,Shangwe Kimath akitoa neno wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Ngassa Mboje akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Iselamagazi wakiimba na kucheza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa Oktoba 11,2017.

Mtoto akiwa ameshikilia bango lililobeba ujumbe.

Awali Watoto wakiandamana na mabango wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa kike.

Watoto wakiwa wameshikilia bango.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal (CCM) akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa kike ambapo aliwasihi wazazi na walezi kupeleka watoto shule kwa ndiyo urithi pekee unaofaa kwa watoto na kuwataka waache kuozesha watoto kwani wanawanyima haki zao.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal aliwaomba wazazi kuwa karibu na watoto wao ili waweze kuwaeleza matatizo wanayokutana nayo

Wadau wakiwa eneo la tukio.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Azza Hilal akicheza na watoto.

Wananchi wa Iselamagazi wakiwa katika maadhimisho hayo.

Wanafunzi wakicheza muziki.

Wadau kutoka taasisi na mashirika mbalimbali yanayohusika na masuala ya watoto wakiwa eneo la tukio.

Watoto wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa maadhimisho hayo.

Burudani ya Ngoma ya Mabulo ya Jeshi kutoka kundi linaloongozwa na Msanii wa Nyimbo za asili Wanzigiza ikiendelea.

Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia akielezea kuhusu hali ya mimba za utotoni mkoani Shinyanga,ambapo alisema mkoa wa Shinyanga unashika nafasi ya tano kwa mimba za utotoni kwa asilimia 34 ambapo mkoa wa kwanza ni Katavi (45% ,Dodoma (43%),Tabora (39%) na Mara (37%).

Wanafunzi wakiimba kwaya

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike kimataifa yakiendelea.

Watoto wa kiume wakiimba wimbo kuwaasa watoto wa kike kuepuka vishawishi ili watimize ndoto zao.

Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.

Mtoto Rosemary Richard akisoma risala mbele ya mgeni rasmi.

Watoto wakiwa wameshikilia katarasi zenye maandishi yanayoonesha matukio,matendo,mila potofu zinazomkandamiza mtoto wa kike kabla ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuzichoma kama ishara ya kupinga vitendo hivyo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia wakichoma moto katarasi zenye maandishi yanayoonesha matukio,matendo,mila potofu zinazomkandamiza mtoto wa kike.

Karatasi hizo zikiwaka moto.

Wadau wakiwa katika eneo la tukio.

Watoto wakicheza mchezo wa igizo kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.

Meza kuu wakifuatilia kwa umakini igizo la watoto kuhusu mimba na ndoa za utotoni.

Wimbo kutoka kwa wananchi wa Iselamagazi ikiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akipanda mti wa kumbukumbu katika shule ya Msingi Iselamagazi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akipanda mti.

Picha ya pamoja ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro na wadau baada ya kupanda mti.

Walimu wa shule ya msingi Iselamagazi wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya mti uliopandwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.

Wanafunzi wa shule ya msingi Iselamagazi wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka Shirika la Save the Children

Wanafunzi wakifurahia.

Picha ya kumbukumbu.



Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Monday, September 18

Zanzibar arrests 20 over homosexuality



Twenty people have been arrested on Tanzania’s semi-autonomous archipelago of Zanzibar for alleged homosexuality, police said.
The 12 women and eight men were picked up in a hotel where they were receiving training about HIV/AIDS education programmes.
Earlier this year, authorities banned many private health clinics from providing HIV services, saying they encouraged gay sex.
Homosexuality is a crime in Tanzania.
Regional police commander Hassan Ali Nasri said on state television: “They are implicated in homosexuality. We arrested them and are busy interrogating them. The police cannot turn a blind eye to this practice.”
On Friday, Deputy Health Minister Hamisi Kingwangalla vowed in front of parliament to “fight with all our strength against groups supporting homosexuality in our country,” AFP news agency reports.
In July 2016, the government banned the import and sales of sexual lubricants, with Health Minister Ummy Mwalimu saying it encouraged homosexuality which led to the spread of HIV/Aids, AFP added.
Gay male sex is punishable by up to 30 years in jail in the country.
Despite the ban on homosexuality, Tanzania was until recently tolerant toward gay people than many other African countries, but a rise in anti-gay rhetoric by government appears to have led to a spike in discrimination.
In July, human rights group Amnesty International said the authorities were “arresting and prosecuting people on homosexuality-related charges, and subjecting them to forced anal examinations.”
Agencies

Friday, August 4

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI AKIELEKEA TANGA MJINI







Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Mkata wakati alipokuwa njiani kuelekea mkoani Tanga kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Mkata waliosimama pembeni ya barabara kuu ya Chalinze- Segera (hawaonekani pichani) mara baada ya kumaliza kuhutubia katika kijiji cha Mkata mkoani Tanga.

Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Tanga akiwemo Wabunge na wakuu wa Wilaya wakipiga makofi wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia Mkata mkoani Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa waliosimama pembeni ya barabara kuu ya Chalinze Segera katika eneo la Kwa mkonga wakati akiwa njiani kuelekea Tanga.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Kabuku mara baada ya kumaliza kuwahutubia wakati akielekea mkoani Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kabuku Handeni mkoani Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela kabla ya kuwahutubia wananchi wa Hale mkoani Tanga.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Hale mkoani Tanga.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja ya wakazi wa Hale mkoani Tanga mara baada ya kuhutubia katika eneo hilo.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Hadija Juma mara baada ya kusoma ujumbe ulioandikwa kwenye sare aliyovaa mama huyo.




Wananchi wa Muheza wakimpokea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kufika katika eneo hilo la mjini akiwa njiani kuelekea Tanga. PICHA NA IKULU.