We capture your memories forever.

Showing posts with label Pictures. Show all posts
Showing posts with label Pictures. Show all posts

Thursday, September 28

WATANZANIA WAMETAKIWA KUENZI UTAMADUNI WETU KUKUZA FURSA ZA UTALII WA KIUTAMADUNI

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbulu

Watanzania wametakiwa kuenzi mila na desturi ambazo ni chanya wazitunze na kuzitumia ili kujenga jamii yenye maadili mema nchini kwa manufaa ya kizazi cha sasa na baadaye.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipotembelea Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom wilaya Mbulu mkoani Manyara ambapo amejionea utajiri wa kiutamaduni wenye fursa za utalii wa kiutamaduni.

“Nimetembelea nyumba za asili zilizopo hapa katika kituo hiki nimefurahishwa sana na utajiri wa kiutamaduni uliopo hapa, wazee walizingatia maadili katika kuwalea watoto wao kulingana na mila na desturi zao, ni vema tuenzi utamaduni wetu, huo ni msingi wa maadili mema ya jamii” alisema Naibu Waziri Wambura

Akitolea mfano wa maadili mema yanayopaswa kurithishwa aliyojionea katika kituo cha 4CCP na namna ambavyo watoto waliheshimu nyumba za wazazi wao, Naibu Waziri Wambura amesema kuwa kwa mujibu wa mila na desturi za Kitanzani suala la ulevi na utumiaji wa tumbaku kwa vijana ilikuwa ni mwiko hadi kijana afikie umri wa utu uzima ambapo anaweza kuwa na maamuzi sahihi katika maisha yake yenye kuwa na tija kwa familia.

“Kabla ya kuoa kijana alikuwa haruhusiwi kutumia tumbaku na kunywa pombe, bali kijana akioa na kuwa na watoto wawili kwa mujibu wa mila za makabila ya yaliyopo Mbulu aliruhusiwa kuingia katika kundi la watu wazima na kuruhusiwa kutumia vitu mbalimbali ikiwemo tumbaku na kinywaji cha pombe. Hapa kuna jambo la Watanzania kujifunza na kutunza ili kuondokana na mmomonyoko wa maadili” alisema Naibu Waziri Wambura.

Mila za jamii zilizo njema zinapaswa kutunzwa na kuendelezwa ili ziweze kusaidia vijana na jamii kwa ujumla kuweka mawazo yao katika shughuli za maendeleo pamoja na kupatia familia zao mahitaji ya kila siku.

Naibu Waziri Wambura alisisitiza kuwa mila hizo hazitakiwi kuachwa bali zainatakiwa kuenziwa, kutunzwa, kuendelezwa na kuhifadhiwa kwa manufaa ya sasa ziweze kuchangia katika kukuza utalii wa kiutamaduni ambao ni moja ya vyanzo vya mapato kwa wanajamii na taifa kwa ujumla.

Aidha, Naibu Waziri Wambura alisema kuwa wilaya ya Mbulu ni tajiri katika masuala ya utamaduni na kuongeza kuwa wilaya hiyo ni mdau muhimu katika sekta ya michezo na utamaduni ambazo zinapaswa kuendelezwa kwa manufaa ya taifa.

Kwa upande wake Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay amesema kuwa wilaya hiyo imekuwa na utamaduni wa kufanya tamasha la utamaduni kila mwaka ambapo mwaka huu lilifanyika tarehe 21 hadi 23 mwezi Septemba na inaedelea kuimarisha umoja, mshikamano na ushirikiano miongoni mwa jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo hatua inayopelekea makabila yote kuwa mstari wa mbele katika kudumisha amani ya nchi.

Mbunge huyo aliyataja makabila yanayotokana na makundi makuu manne yanayopatikana wilaya ya Mbulu kuwa ni pamoja na Wairaqw ambao ni jamii ya Wakushi, Wahadzabe jamii ya Khoisan, Wanyiramba na Wanyisanzu jamii ya wabantu na Wadatooga jamii ya Kiniloti.

Naye Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga amemhakikishia Naibu Waziri Wambura kuwa wilaya hiyo itaendelea kuenzi sekta ya utamaduni kwa kuwa na tamasha la utamaduni linalokutanisha makabila yote wilyani humo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uanuwai wa Utamaduni duniani ambayo hufanyika mwezi Mei tarehe 21 kila mwaka.

Hatua hiyo inatokana na Tanzania kusaini mkataba wa azimio la Umoja wa Mataifa (UN) kuenzi utamaduni na kuheshimu tamaduni za watu wengine chini unaosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Mwaka 2002 Umoja wa Mataifa uliamua kuanzisha maadhimisho ya siku ya Utamaduni Duniani kutokana na kuongezeka kwa migogoro, mapigano na kupotea kwa maisha ya watu na mali zao iliyokuwa inatokea sehemu mbalimbali duniani mwishoni mwa miaka ya 1990.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa pili kushoto) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi na Usalama mara baada ya kuwasili Wilayani Mbulu kwa ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani humo.

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura kuongea na wananchi waliokuwa katika tamasha la utamaduni katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom mara baada ya kuwasili Wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani humo.

Baadhi ya Washiriki wa tamasha la utamaduni katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) Haydom, wilaya ya Mbullu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (hayupo pichani) alipotembelea kituo hicho.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akitoka ndani kujionea moja ya nyumba za asili ya Wabantu Wanyiramba na Wanyisanzu iliyopo Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akicheza ngoma na washiriki wa tamasha la utamaduni alipotembelea Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa pili kulia) akipata maelezo ya utamaduni wa kabila la Wadatoga katika Kituo cha Pembe Nne za Utamaduni (4CCP) kilichopo Haydom.

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wasichana wa kabila la Datoga na kusisitiza Watanzania kuenzi utamaduni wetu kwa kuurithisha kwa vijana wetu. Wa nne kushoto ni Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay.(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbulu)

Friday, September 1

Kim Kardashian shows off her perfectly toned body in new photo

The reality star and mother of two showed off her perfectly toned body in a bikini photo she shared on her Instagram page. She captioned; "It's really hot today"

Wednesday, August 30

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AZINDUA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI MAGEREZA, GEREZA KUU ARUSHA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Mkoani Arusha alipowasili katika viwanja vya Gereza Kuu Arusha katika ziara Maalum ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha leo Agosti 28, 2017 ambapo nyumba hizo zimejengwa hivi karibuni na Uongozi wa Jeshi hilo kwa kutumia fedha iliyopatikana katika miradi ya Shirika la Magereza. Kushoto kwa Waziri ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha, leo Agosti 28, 2017(Wa pili kulia) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kulia) ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mhe. Gobless Lema.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kutoa hotuba fupi ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akitoa hotuba mbele ya Maofisa na askari wa Magereza Mkoani Arusha katika hafla ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(katikati) akikagua nyumba za askari Magereza zilizojengwa kwa kutumia fedha iliyopatikana katika miradi ya Shirika la Magereza(kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Khamis Nkubasi.

Muonekano wa nyumba zilizozinduliwa za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.

Baadhi ya Maafisa na Askari wa Magereza Mkoani Arusha waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akimpongeza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Khamis Nkubasi mara baada ya uzinduzi wa nyumba hizo(katikati) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo(kulia) alipomtembelea ofsini kwake leo kabla ya uzinduzi rasmi wa nyumba za makazi ya askari wa Gereza Kuu Arusha.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na Askari ambao ni mafundi ujenzi waliojenga nyumba hizo(waliosimama) mara baada ya hafla ya uzinduzi wa nyumba hizo. Wengine walioketi ni Kamishna Jenrerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa tatu toka kushoto), wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mhe. Gobless Lema(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Tuesday, August 8

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOHITIMISHA ZIARA YAKE YA KIKAZI YA SIKU TANO MKOANI TANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzirasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji wa Korogwe mkoani Tanga katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza madiwani na viongozi wengine baada ya kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi baada ya kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akienda kuagana na wananchi baada ya kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mmoja wa wa wananchi baada ya kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Moja ya mabango yaliyokuwa na ujumbe wa changamoto mbalimbali za Korogwe

Wengi walikuwa na kiu ya kusikilizwa kero zao

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza diwani wa kata ya Msima katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Wananchi wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama kwa muda na kuongea nao katika kata ya Msima katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Kikosi kazi cha TBC kikirusha mubashara matukio yote ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Hapa ni katika Msima katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulisha viongozi alioongozana nao kwa wananchi wa kata ya Msima katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsimiliza mwalimu wa shule ya msingi ya Msima aliposimama kuzungumza na wananchi kata ya Msima katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella akielezea changamoto mbalimbali za wananchi wa kata ya Msima katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi shilingi milioni 5 taslimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi ya Msima kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukiingia mjini Handeni katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika nyumba ya aliyekuwa Mbunge wa Handeni Marehemu Alhaj Dkt. Abfdallah Kigoda katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Tanga leo Agosti 7, 2017. Pamoja naye ni mjane wa marehemu Mama Kigoda, dada wa Marehemu Mhe, Asha Kigoda na mtoto wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Omari Abdallah Kigoda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli waakitoa heshima zao kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Handeni Marehemu Alhaj Dkt. Abfdallah Kigoda nyumbani kwa marehemu mjini Handeni katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Tanga leo Agosti 7, 2017. Pamoja naye ni mjane wa marehemu Mama Kigoda, dada wa Marehemu Mhe, Asha Kigoda na mtoto wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Omari Abdallah Kigoda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe alipowasili wilayani humo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akipungia wanannchi alipowasili katika uwanja wa mikutano wa Kibaoni kuzungumza nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwakipungia wananchi wa Handeni alipowasili katika uwanja wa mikutano kuzungumza nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia wananchi alipowasili katika uwanja wa mikutano kuzungumza nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia viongozi wa dini na wananchi alipowasili katika uwanja wa mikutano kuzungumza nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akikaribisha wageni wake wilayani humo katika siku ya mwisho ya ziara Rais ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Sehemu ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa mikutano alipofika kuzungumza nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimia wananchi wa Handeni katika uwanja wa mikutano kuzungumza nao katika siku ya mwisho ya ziara ya Rais ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Handeni katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Sehemu ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa mikutano alipofika kuzungumza nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Sehemu ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa mikutano alipofika kuzungumza nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akitolea ufafanuzi baadhi ya changamoto wilayani humo leo Agosti 7, 2017

Mmoja wa wananchi wa Handeni akitoa kero zake mbele ya Rais Magufuli

Rais Magufuli akimfariji mwananchi huyo kwa matatizo yaliyomsibu

Mmoja wa wananchi wa Handeni akitoa kero zake mbele ya Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuliakiagana na viongozi na wananchi wa Handeni baada ya kuwahutubia katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Msafara wa Rais Magufuli ukiendelea na safari

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi wa Manga aliposimama kwa muda kuongea nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

Mbunge wa Handeni Vijijini Mhe. Mboni Mhita akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali wakati Rais Magufuli aliposimama kwa muda katika kijiji cha Kwachaga

Mafundi mitambo wa TBC wakiwa makini kuhakikisha matangazo yanaruka mubashara bila shida

Mkulima wa kijiji cha Manga akieleza kero wazipatazo kwa wafugaji katika kata ya Kwachuma

Mmoja wa viongozi wa wafugaji akifafanua hali ilivyo kata ya Kwachuma

Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akitoa maelezo ya changamoto mbalimbali katika kata ya Kwachuma

Rais Dkt. Magufuli akiagiza kuondolewa kwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Mazingara baada ya wananchi na Mkuu wa Wilaya kudai amekuwa akitoa uamuzi usiotoa haki kwa wakulima

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella akimuaga rasmi Rais Dkt. Magufuli na kumshukuru kwa kutembelea mkoa huo kwa siku tano

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimia wananchi wa kata ya Kwachuma

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimia wananchi wa kata ya Kwachuma

Rais Dkt. Magufuli akiaga wananchi wa kata ya Kwachuma

Rais Dkt. Magufuli akiagana na viongozi wa mkoa wa Tanga baada ya kuongea na wananchi wa kata ya Kwachuma

Kabla ya kuondoka Rais Dkt. Magufuli aliongea na wanafunzi wa shule za kata ya Kwachuma

Rais Dkt. Magufuli akiongea na wanafunzi wa shule za kata ya Kwachuma

Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza mwanafunzi Mwajuma Omari Mbwewe
Rais Dkt. Magufuli akijibu maswali ya mwanafunzi huyo wa shule za kata ya Kwachuma

Rais Dkt Magufuli akiagana na mwanafunzi Mwajuma Omari Mbwewe baada ya kujibu maswali yake

Akiwa njiani msafara wa Rais Dkt. Magufuli ulisimamishwa na umati mkubwa wa watu maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam ambapo ikambidi asimame na kuongea nao

Umati mkubwa wa watu maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam ambapo ukimsikiliza Rais Magufuli

Rais Dkt. Magufuli akiongea na umati mkubwa wa wananchi uliomsimamisha maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam

Rais Dkt. Magufuli akisikiliza kero za wafanyabiashara wadogo maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam

Kama kawaida ujumbe ulikuwepo

Rais Dkt. Magufuli akimfariji mmoja wa wafanyabiashara wadogo waliopata changamoto eneo la Bunju A

Rais Dkt. Magufuli akishangiliwa na umati wa wananchi uliomsimamisha maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam

Rais Dkt. Magufuli akiagana na umati wa wananchi uliomsimamisha maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam

Rais Dkt. Magufuli akiagana na umati wa wananchi uliomsimamisha maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Picha na IKULU