We capture your memories forever.

Thursday, June 22

Prof. Maghembe Amuaga Egon Konchane



Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Waziri Maghembe alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano na misaada mbalimbali aliyoitoa, yeye binafsi na nchi yake katika kusaidia kuendeleza sekta ya uhifadhi nchini.

Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (katikati) akifurahia zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori alivyopewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi. Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki.

Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous mkoani Morogoro.
Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kulia) akimkabidhi Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe zawadi ya picha ya kumbukumbu ambayo ilipigwa wakati wawili hao wakitua kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Matambwe, Selous, Kwa mujibu wa balozi huyo siku hiyo haikuwa rahisi kwa ndege hiyo kutua kwa kuwa mvua zilikuwa zinanyesha. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

No comments:

Post a Comment