We capture your memories forever.

Friday, September 1

Young D Aomba Radhi kwa Picha zinazosambaa mitandaoni




Rapper Young Dee ameomba radhi baada ya picha tata akiwa na Amber Lulu kusambaa mtandaoni. Kwenye picha hiyo, Young anaonekana akikodolea macho makalio ya video vixen huyo aliyegeukia muziki. Amber yuko nusu utupu.
Kupitia Instagram, Young Dee ameandika:
Nasikitishwa kwa picha inayosambaa mitandaoni.. imevuja bila ridhaa yangu ni picha iliyokua imepigwa behind the scene lengo haswa la photoshoot ni aina hii mpya ya mavazi ya aina ya ki"Scortish" kama sketi. Naomba radhi sana kwa hili! Na kwa mashabiki wote!😒 So sad!
Pamoja na kuomba radhi, bado mashabiki wanamshambulia rapper huyo kwa vazi hilo lenye sketi.

No comments:

Post a Comment